Machapisho maarufu kutoka blogu hii
MUGABE APEWA MASAA KUJIUZULU
Baada ya kuvuliwa nafasi ya kiongozi wa juu wa Chama cha Zanu- PF Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepewa masaa tu na Chama hicho kujiuzulu mwenyewe kwenye nafasi ya Urais wa nchi hiyo bila kutumia nguvu. Chama tawala nchini humo leo baada ya kutangaza kuwa kimemvua uongozi Rais huyo mkongwe zaidi barani Afrika, Robert Mugabe, kimemwambia hadi kesho saa 6 mchana awe tayari ametangaza kujiuzulu nafasi ya Urais huku kikimuonya kuwa endapo atakaidi nguvu ya ziada itatumika kumng’oa madarakani. “ Rais wetu wa zamani, Robert Mugabe amepewa muda hadi kesho jumatatu saa 6 mchana awe ameshatangaza kujiuzulu nafasi ya Urais wa Zimbabwe la sivyo nguvu itatumika kumng’oa madarakani .” chama cha Zanu-PF kimeeleza kwenye ukurasa wao rasmi wa Twitter. Nafasi ya Rais Mugabe itachukuliwa na kiongozi mkuu wa Chama tawala cha Zanu PF aliyechaguliwa leo kwenye kamati kuu ya chama hicho,Emmerson Dambudzo Mnangagwa ambaye pia alishawahi kuwa Makamu wa Rais wa Mugabe kabla ya kutimuliwa



















Maoni
Chapisha Maoni