Machapisho

MAMA SAMIA SULUHU AZINDUA MRADI IRINGA

Picha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi. Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima . Makamu wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018. Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato k...

MSUVA APIGA HAT TRICK NDANI YA BEN AHMED EL ABDI

Picha
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Saimon Happygod Msuva usiku wa Jana amelichungulia Mara tatu lango la Benfica ya Guinea Bissau kwenye michuano ya klabu bingwa barani afrika. Ikiwa ni mchezo wa kwanza kwenye mzunguko wa kwanza, Difaa Hassan El Jadida iliibuka na ushindi wa mabao 10-0 katika uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El-jadida, Mazghan Morocco, Msuva alifunga magoli yake dakika ya 44,72 na 88.  Mabao mengine ya Difaa Hassan El Jadida yalifungwa na Bakary N'diaye dakika ya nne, Hamid Ahadad dakika za 23, 26, 37, 42 na 47 na Bilal El Magri dakika ya 54. Sasa akina Msuva watakwenda ugenini Guinea Buissau katika mchezo mwepesi kabisa baada ya ushinsi huo mnono wa nyumbani.

Nyota ya Olunga yang'aa La Liga

Miaka mitatu iliyopita alikuwa tanzania na timu yake ya Gor Mahia iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kagame Cup ilikuwa ni mwaka 2015 ambapo aliisaidia klabu yake kucheza fainali na kupoteza kwa Azam ambao walitangazwa mabingwa wa michuano hiyo ambayo haijafanyika tena tangu mwaka huo, huyu si mwingine bali ni mshambuliaji mrefu raia wa Kenya Michael Olunga. Olunga ameweka rekodi ya kuwa mkenya wa kwanza kufunga ha-trick kwenye ligi ya Hispania La Liga, aliingia akitokea kwenye benchi kuchukua nafasi ya Cristhian Stuani, aliingia wakati timu inaongoza kwa goli 1-0 akaisaidia kushinda kwa magoli 6-0 dhidi Las Palmas. Licha ya kufunga magoli matatu, Olunga alitoa pasi ya mwisho ‘assist’ kwa hiyo amehusika katika magoli manne kati ya sita ambayo Girona wamefunga. Hat-trick yake ilikuwa ya muda mfupi kwa wachezaji ambao wametokea benchi, alitumia dakika 22 kufunga magoli yote matatu, alifunga magoli yake dakika ya 57, 70 na 79. Kwa sasa Olunga yupo Girona FC kwa mkopo akitokea China...

Front page za magazeti ya leo tr 13 Jan,2018

Picha

KWASI AANZA KUPIGA TIZI MSIMBAZI LEO ASUBUHI

Picha
Beki huyo ambaye alikua akiichezea lipuli amesema anajitambua kama mchezaji wa simba na Leo asubuhi ataungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ndani ya kambi ya polisi. Licha ya mabosi wake wa wa zamani lipuli wakiendelea kusisitiza kuwa Kwasi bado ni mali yao na watashangaa simba wakimtumia kwa sasa, yeye ameamua kuanza mazoezi na klabu ya simba Leo jumatatu. "Mimi ni mchezaji wa simba baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili na klabu ya simba na suala linalolalamikiwa lishamalizwa na meneja wangu" alisema beki huyo wa kati.

MSUVA AZIDI KIJIONGEZEA UMAARUFU MOROCCO

Picha
BAO pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva limeipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El Jadida dhidi ya Kawkab Marrakech katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida. Msuva alifunga bao hilo dakika ya 55 huo ukiwa mwendelezo wake wa kufanya vizuri katika klabu yake ya Kaskazini mwa Afrika na Ligi ya Morocco kwa ujumla. Pamoja na hayo, Msuva alipumzishwa dakika za mwishoni ili awe fiti zaidi kwa ajili ya mchezo ujao, nafasi yake akiingia Adnane El Ouardy dakika ya 85. Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida imefikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 12 na kuendelea kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 23 za mechi 12 pia. Source:  Bin Zubery

SUALA LA UWAKILISHI KWA MAZOEA TAIFA STAR LIANGALIWE KWA UMAKINI

Picha
Waziri wa michezo Dr. Herrison Mwakyembe amesema suala la kuita wachezaji kuwakilisha timu ya taifa limekuwa la mazoea. “ Sasa uwakilishi kwenye timu Taifa Stars kwa mazoea, hili suala lazima tuliangalie kwa makini sana. Sio mchezaji anakuwa anauhakika wa kuitwa kwenye timu, tunataka tuone kwa kujituma ” alisema mwakyembe. Pia waziri Mwakyembe amesema kuwa vijana wa Zanzibar Heroes wanavyojiyuma lazima warudi na kombe la challenge cup 2017, kitu ambacho kitawafurahisha watanzania.  "MUNGU AWATANGULIE Z'BAR HEROES KWENYE FAINALI YA CHALLENGE CUP"