SUALA LA UWAKILISHI KWA MAZOEA TAIFA STAR LIANGALIWE KWA UMAKINI
Waziri wa michezo Dr. Herrison Mwakyembe amesema suala la kuita wachezaji kuwakilisha timu ya taifa limekuwa la mazoea.
“Sasa uwakilishi kwenye timu Taifa Stars kwa mazoea, hili suala lazima tuliangalie kwa makini sana. Sio mchezaji anakuwa anauhakika wa kuitwa kwenye timu, tunataka tuone kwa kujituma” alisema mwakyembe.
Pia waziri Mwakyembe amesema kuwa vijana wa Zanzibar Heroes wanavyojiyuma lazima warudi na kombe la challenge cup 2017, kitu ambacho kitawafurahisha watanzania.
"MUNGU AWATANGULIE Z'BAR HEROES KWENYE FAINALI YA CHALLENGE CUP"

Maoni
Chapisha Maoni