MSUVA APIGA HAT TRICK NDANI YA BEN AHMED EL ABDI


Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Saimon Happygod Msuva usiku wa Jana amelichungulia Mara tatu lango la Benfica ya Guinea Bissau kwenye michuano ya klabu bingwa barani afrika.
Ikiwa ni mchezo wa kwanza kwenye mzunguko wa kwanza, Difaa Hassan El Jadida iliibuka na ushindi wa mabao 10-0 katika uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El-jadida, Mazghan Morocco, Msuva alifunga magoli yake dakika ya 44,72 na 88. Mabao mengine ya Difaa Hassan El Jadida yalifungwa na Bakary N'diaye dakika ya nne, Hamid Ahadad dakika za 23, 26, 37, 42 na 47 na Bilal El Magri dakika ya 54.Sasa akina Msuva watakwenda ugenini Guinea Buissau katika mchezo mwepesi kabisa baada ya ushinsi huo mnono wa nyumbani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MUGABE APEWA MASAA KUJIUZULU