MSUVA AZIDI KIJIONGEZEA UMAARUFU MOROCCO
BAO pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva limeipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El Jadida dhidi ya Kawkab Marrakech katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida.Msuva alifunga bao hilo dakika ya 55 huo ukiwa mwendelezo wake wa kufanya vizuri katika klabu yake ya Kaskazini mwa Afrika na Ligi ya Morocco kwa ujumla.Pamoja na hayo, Msuva alipumzishwa dakika za mwishoni ili awe fiti zaidi kwa ajili ya mchezo ujao, nafasi yake akiingia Adnane El Ouardy dakika ya 85.Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida imefikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 12 na kuendelea kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 23 za mechi 12 pia.Source: Bin Zubery

Maoni
Chapisha Maoni