AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUUA
Mkazi wa Ipililo wilaya ya Maswa Mkoani Shinyanga, Salum Nkoja (22) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Kisutu akikabiliwa na kosa la mauaji ya kukusudia ya mtu asiyefahamika.Hata hivyo, kwa taarifa zilizoko inadaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na viungo vya binadamu zikiwemo sehemu za siri wanawake. Mshtakiwa alisomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.
Maoni
Chapisha Maoni