Kibatala aelezea kuhusu hukumu ya Lulu


Peter Kibatala, wakili wa Elizabeth 'lulu' kupitia akaunti yake ya instegram amefafanua kuhusu hukumu ya lulu kuwa kuna uwezekano was kukata rufaa.

Amesema kuwa hakuna hukumu tofauti inayoweza kutolewa kabla mhukukiwa hajatumikia theluthi ya kufungo chake ambacho kwa Lulu itakuwa ni kuanzia miezi mitano.Ndani ya hiyo miezi mitano dhamana inaweza kuombwa wakati wakisubiria rufaaa ianze kusikilizwa. Kwa maana hiyo anaweza kutoka kwa dhamana muda wowote mahakama ikimpatia dhamana.Huwezi kuacha kijana wa miaka 22 mwenye maisha marefu mbele yake ahukumiwe kwa uhalifu kwa sababu ya suala la muda, kwani itaharibu maisha yake ya mbele. Kwa hiyo rufaa imelenga katika kuondoa tatizo hilo.Kukata rufaaa na kuomba dhamana na kufanya kazi za jamii vinaweza kufanyika kwa wakati mmoja wakati suala hili likisubiriwa kusikilizwa na mahakama ya rufaa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MUGABE APEWA MASAA KUJIUZULU