MAHAKAMA YA RUFAA YAMMINYA OSCAR PIOSTOTIUS
Oscar Pistorius ameongezewa adhabu ya kifungo kutoka miaka 6 na kuwa miaka 13 na miezi mitano na mahakama ya rufaa nchini Afrika kusini. Pistorius alihukumiwa kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kukusudia.
Hatua hii inafuatia madai kutoka upande wa serikali kwamba adhabu aliyopewa awali ya miaka sita ilikuwa ndogo.Pistorius alishtakiwa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi 4, katika siku ya wapendanao mwaka 2013, na baadaye Pistorious alisema alifyatua risasi hizo kwa kujua ni mwizi.

Maoni
Chapisha Maoni