MAMIA WAUAGA MWILI WA NDIKUMANA
Wananchi wa Rwanda pamoja na wapenzi wa soka wa Afrika Mashiriki siku ya jana walipokea kwa mshituko mkubwa kifo cha ghafla cha aliyekuwa kapteni wa timu ya Taifa ya Rwanda, Hamad Ndikumana ambaye pia alikuwa ni mume wa muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya.
Umati wa watu umejitokeza kwenye msikiti wa Qaddafi huko Nyamirambo Rwanda kwa ajili ya kumuaga mwanasoka huyo mkongwe.
Ndikumana anadaiwa kufariki dunia mda mchache baada ya kutoka mazoezini akiwa kama kocha was timu ya Rayon sport. Marehemu alikua na mtoto mmoja aliezaa na mwigizaji wa bongo movie Iren uwoya.

Maoni
Chapisha Maoni