Michoro ya watoto kutoka Tanzania wazawadiwa Finland.

Pichani ni watoto waliopata tuzo.
Michoro mitatu iliyochorwa na watoto kutoka Tanzania hivi karibuni ilitunukiwa tuzo ya heshima ya vyeti vya stashahada ya maonesho na Taasisi ya Sanaa za watoto na vijana ya Hyvinkää, Finland.Bryton Manyewa(10), Neev Mistry (9) wa shule ya Academic International Primary na Mandela Mtaya (5) wa shule ya chekechea ya Upendo Montessori ndiyo waliofanikiwa kupata tuzo hiyo kwa upande wa Tanzania baada ya kushiriki shindano la michoro liloitwa 'Pamoja' lililotayarishwa na taasisi hiyo ya nchini Finland.

Maoni
Chapisha Maoni