PROF. KITILA AREJEA CCM
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kuwa amejiunga tena na chama hicho.
Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Mkoani Singida, Bi. Martha Mlata imesema chama hicho Mkoa wa Singida wanamkaribisha kwa mikono miwili ili waendelee kuimarisha chama katika mkoa huo.
Huku Mlata akielezea jinsi alivyorudi kwenye chama chake cha zamani amesema nina furaha kuwatangazia wanachama na wapenzi wa CCM Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujuma kuwa, Profesa Kitila Mkumbo amejiunga tena na chama chetu, Ni fursa kubwa kwa mkoa kumpokea mwalimu baada ya kumpoteza mwanafunzi siku chache zilizopita.
Profesa Mkumbo amejiunga wiki moja iliyopita na amelipia ada yote aliyokuwa akidaiwa katika kipindi chote na mimi nilichokifanya ni kuwajulisha tu wanachama wetu kuwa mwana mpotevu karudi nyumbani.

Maoni
Chapisha Maoni