STRAIKA wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa ameendelea 'kung'ara' katika Ligi Kuu Bara baada ya kufunga 'Hat -trick' yake ya kwanza msimu huu kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City, leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mabao mawili yakifungwa na Emmanuel Martin.
Chirwa aliwaamsha mashabiki dakika ya 20 kipindi cha kwanza, Emmanuel Martin naye hakuchelewa akatupia bao la pili dakika ya 23. Na mabao mengine ya chirwa aliyafunga dakika ya 50 na 59 na Emmanuel Martin akafunga dimba kwa kufunga bao la mwisho dakika ya 80.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MUGABE APEWA MASAA KUJIUZULU