FAMILIA YA BABU SEYA KUWA HURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli Leo tarehe 9/12/2017 kwenye maathimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania ametoa tamko la kuiachia huru familia ya mwanamziki nguli hapa nchini Nguza Viking maarufu kama babu seya.

Nguza Viking (babu seya ) pamoja na Jonson Nguza (papii kocha) wamepata msamaha huo baada yakutumikia sehemu ya hukumu yao baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha miaka kadhaa iliyopita. Pia Rais Dkt. Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 ambapo wafungwa 1828 wataachiwa huru leo na 6329 wamepunguziwa muda wa kifungo chao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MUGABE APEWA MASAA KUJIUZULU