Mwanasheria David Nzarigo atiwa mikononi mwa serikali
Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.
Maoni
Chapisha Maoni