Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2017

KWASI AANZA KUPIGA TIZI MSIMBAZI LEO ASUBUHI

Picha
Beki huyo ambaye alikua akiichezea lipuli amesema anajitambua kama mchezaji wa simba na Leo asubuhi ataungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ndani ya kambi ya polisi. Licha ya mabosi wake wa wa zamani lipuli wakiendelea kusisitiza kuwa Kwasi bado ni mali yao na watashangaa simba wakimtumia kwa sasa, yeye ameamua kuanza mazoezi na klabu ya simba Leo jumatatu. "Mimi ni mchezaji wa simba baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili na klabu ya simba na suala linalolalamikiwa lishamalizwa na meneja wangu" alisema beki huyo wa kati.

MSUVA AZIDI KIJIONGEZEA UMAARUFU MOROCCO

Picha
BAO pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva limeipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El Jadida dhidi ya Kawkab Marrakech katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida. Msuva alifunga bao hilo dakika ya 55 huo ukiwa mwendelezo wake wa kufanya vizuri katika klabu yake ya Kaskazini mwa Afrika na Ligi ya Morocco kwa ujumla. Pamoja na hayo, Msuva alipumzishwa dakika za mwishoni ili awe fiti zaidi kwa ajili ya mchezo ujao, nafasi yake akiingia Adnane El Ouardy dakika ya 85. Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida imefikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 12 na kuendelea kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 23 za mechi 12 pia. Source:  Bin Zubery

SUALA LA UWAKILISHI KWA MAZOEA TAIFA STAR LIANGALIWE KWA UMAKINI

Picha
Waziri wa michezo Dr. Herrison Mwakyembe amesema suala la kuita wachezaji kuwakilisha timu ya taifa limekuwa la mazoea. “ Sasa uwakilishi kwenye timu Taifa Stars kwa mazoea, hili suala lazima tuliangalie kwa makini sana. Sio mchezaji anakuwa anauhakika wa kuitwa kwenye timu, tunataka tuone kwa kujituma ” alisema mwakyembe. Pia waziri Mwakyembe amesema kuwa vijana wa Zanzibar Heroes wanavyojiyuma lazima warudi na kombe la challenge cup 2017, kitu ambacho kitawafurahisha watanzania.  "MUNGU AWATANGULIE Z'BAR HEROES KWENYE FAINALI YA CHALLENGE CUP"

RAISI MSTAAFU KIKWETE AIPONGEZA ZANZIBAR HEROES

Baada ya timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kufuzu kucheza fainali ya michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup 2017, Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Dr. Jakaya Kikwete ‘JK’ ametuma salam za pongezi kwa timu hiyo. Kupitia ukurasa wake wa twitter JK ameandika: “Nawapongeza Zanzibar Heroes kwa kututoa kimasomaso na kutinga fainali. Nawatakia kila la kheri katika mechi ya fainali waibuke na kombe na watupe raha ambayo Watanzania tumeikosa kwa muda mrefu.” Zanzibar waliifunga 2-1 timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ kwenye mchezo wa nufu fainali, ikumbukwe Uganda ndio walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo walilolitwaa mwaka 2015. Mwaka huohuo Uganda waliifunga Zanzibar 4-0 katika mchezo wa hatua ya makundi. Mchezo wa fainali utachezwa Jumapili December 17, 2017 kati ya wenyeji Kenya dhidi ya Zanzibar. Source:  Shaffih Dauda

WACHEZAJI WAWILI WAFUNGA USAJILI YANGA

Yanga imehitimisha usajili wake kwenye dirisha dogo kwa kumsajili beki mkongoman Fistoo Kayembe na mshambuliaji Yohana Mkomola. Hussein Nyika mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga amesema kuwa usajili wao umefikia mwisho kwa kuwasajili wachezaji wawili pekee. "Tulipanga kufanya usajili mkubwa lakini muda umekuwa mfupi lakini pia kama mnavyojua usajili sio kitu cha kukurupuka tulisema tunatafuta  kiuongo tukamleta Pappy (Tshishimbi) watu wakarithika, tulisema tunatafuta mshambuliaji tukamleta Hajibu watu wakafurahia pia. Hivyo tulitaka kufanya kweli lakini tukakosa kile tulichotaka ndo mana tukafanya usajili huu" alisema Nyika.

CANNAVARO 'BADO NAFASI YA KUTETEA UBINGWA IPO'

Picha
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'cannavaro' amesema licha ya watani wao wa jadi kuongoza ligi bado nafasi ya kutete ubingwa ipo. Cannavaro amesema kuwa Simba imeipita Yanga kwa alama mbili ambazo haziwezi kuwakwamisha kwenye mbio za kutetea ubingwa punde tu mzunguko wa pili utakapoanza. Nahodha na beki huyo wa Yanga amesema wapo kwenye mazoezi ambayo yatakamilika zaidi wachezaji wenzake waliopo kwenye kombe la chalenji watakaporudi.

WIZI WA MAFUTA YA TRENI TAZARA WAKERA POLISI

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Tazara, Patrick Byatao amesema wafanyakazi wasio waaminifu wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) wanalisababishia hasara shirika hilo kutokana wizi wa mafuta katika treni. Akizungumza katika hafla ya kuwapa zawadi wafanyakazi bora 10 wa mwaka 2017, Dar es Salaam jana, Kamanda Byatao aliyataja maeneo korofi ambayo wizi huo hufanyika kuwa ni pamoja na stesheni ya Mlimba (Kilombero), Makambako (Njombe), Kongaga (Mbarali), Mpemba (Songwe) na Tunduma. Alisema watumishi hao hususani madereva wamekuwa wakishirikiana na wananchi kuiba mafuta na ndiyo maana shirika hilo haliendelei. Kamanda Byatao alisema kuwa Oktoba 7, mwaka huu, walifanikiwa kumkamata dereva wa treni, Kagwa Ruoga na Mathew Mkula ambao walikuwa wakiendesha treni lililobeba shaba kutoka Zambia kwenda Dar es Salaam na kwamba huku treni hilo likiwa linatembea waliingiza watu watano na kuanza kuchukua mafuta ya dizeli. Aliwataka wananchi kutoshiriki katika matukio hayo ya uhalifu na kwamba ...

BARCELONA YAMUWINDA BLIND

Picha
Barcelona inataka saini ya mchezaji kiraka Daley Blind wa Manchester United ambaye mkataba wake Man united umebakia miezi sita. Blind anaweza kucheza nafasi ya beki na kuingo mkabaji, na mchezaji huyo anaweza asisaini mkataba mpya kwa kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza Man United. Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde anamuwinda kiraka huyo mwenye umri wa miaka 27 kwenye msimu ujao wa kiangazi

Mwanasheria David Nzarigo atiwa mikononi mwa serikali

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali . Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira . Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.

FAMILIA YA BABU SEYA KUWA HURU

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli Leo tarehe 9/12/2017 kwenye maathimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania ametoa tamko la kuiachia huru familia ya mwanamziki nguli hapa nchini Nguza Viking maarufu kama babu seya. Nguza Viking (babu seya ) pamoja na Jonson Nguza (papii kocha) wamepata msamaha huo baada yakutumikia sehemu ya hukumu yao baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha miaka kadhaa iliyopita.  Pia Rais Dkt. Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 ambapo wafungwa 1828 wataachiwa huru leo na 6329 wamepunguziwa muda wa kifungo chao.

Msuva aendelea kung'ara Morocco

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva amechaguliwa kwenye kikosi cha wachezaji bora wa mwezi wa ligi ya Morocco. Msuva amesema hakutarajia jina lake kama lingekuwemo kwenye orodha ya kikosi cha wachezaji bora wa mwezi, pia amesema huo ni mwanzo mzuri kwake na sasa ameanza kuziota tuzo zinazowaniwa baada ya msimu wa ligi kumalizika

MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI FAHARI ASHIKILIWA NA POLISI

Picha
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inamshikilia mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Fahari iliyopo Goba kwa kosa la kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema jana Jumanne Desemba 5,2017 kuwa mwanafunzi huyo mwenye miaka 17 (jina linahifadhiwa) anayesoma kidato cha tatu alikamatwa jirani na Benki ya CRDB maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam akiwa amevaa sare za JWTZ. Amesema mwanafunzi huyo akiwa amevaa sare alikuwa akivuta sigara hadharani na kufanya vitendo visivyoendana na maadili ya askari. Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano ya awali, kijana huyo alijitambulisha kuwa ni askari kutoka 501KJ Lugalo jijini Dar es Salaam. Amesema baada ya kubanwa alikiri kupata sare hizo kwa rafiki zake na upekuzi ulipofanywa ndani ya begi alilokuwa nalo alikutwa na kofia nyingine moja ya jeshi hilo. Pia, alikutwa na kitambulisho cha mtoto wa askari wa JWTZ Private Gabriel Kiwila wa 501 KJ. Kamanda Mambosasa amesema kitambulish...

WEUSI: TUNATUMIA LUGHA YA KIKUBWA

Picha
Kundi la muziki wa hip hop Bongo, Weusi limesema kilichofanyika katika ngoma zao ‘‘Amsha Dude na Nicome’, ni sanaa/lugha ya kikubwa. Rapper wa kundi hilo Joh Makini amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm walichofanya katika ngoma hizo mbili ni kucheza na maneno bila kukiuka maadili. “Hiyo ni art, sisi tunatumia sanaa, naweza kuongea maneno ambayo kwa lugha nyingine usingeweza kuyatamka kwenye redio lakini kwa sababu natumia sanaa tunaweza jinsi ya kucheza na maneno kufikisha jumbe ambao tunautaka bila kuvunja sheria au kumkwaza mtu yeyote” amesema Joh Makini. Amsha Dude na Nicome pamoja na Yakulevya ni ngoma ambazo kundi hilo wametoa kwa mwaka huu. Source; Bongo5

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA LITAKALOFANYIKA NCHINI URUSI 2018

Picha