Zimbabwe yajitoa michuano ya CECAFA
Chama cha mchezo wa soka nchini Zimbabwe (ZIFA) kimetangaza kujitoa katika kombe la michuano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA ambayo inatarajiwa kuchezwa nchini Kenya kuanzia Desembe 3 hadi 17 mwaka huu. Kupitia mtandao wake wa kijamii ZIFA imesema imeamua kujiengua katika michuano hiyo kufuatia kutotengemaa kwa hali ya kiusalama kwa nchi mwenyeji Kenya. “Kufuatia mashauriano ya kina na wadau wote, Chama cha mchezo wa soka nchini Zimbabwe (ZIFA) kimeadhimia kujitoa katika kushiriki michuano ya CECAFA Chalenji Cup ya mwaka 2017 kutokana nakutotengemaa kwa hali ya kiusalama kwa nchi mwenyeji Kenya, hivyo basi ZIFA imesimamisha maandalizi yote mara moja ya kushiriki kama mgeni mualikwa wa mwaka huu.” Imesema ZIFA “ZIFA inaahidi kujitolea kushiriki katika mashindano yajayo endapo kama hakutakuwa na hali yoyote ya kiashiria cha ukosefu wa usalama. Kujitoa katika mashindano haya si kitu kizuri kwetu, kwa timu, taifa na hata kwa waandaji wa mashindano wenyewe lakini tulihitaji kuf...